Wauzaji wa pombe ya mnazi jijini Mombasa walifanya maandamano siku ya Jumatatu, kupinga kuhangaishwa na maafisa wa usalama.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wachuuzi hao waliokuwa wameandamana na Mbunge wa Nyali Hezron Awiti pamoja na Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga walidai kuwa maafisa wa usalama huwaitisha hongo licha ya wao kufanya vikao na wakuu wa usalama katika kaunti, akiwemo mshirikishi mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa.

"Wauzaji wa mnazi wamekuwa vitega uchumi wa polisi kila uchao. Wamijikenda wanategemea biashara ya mnazi kulisha familia zao na wanachokifanya polisi nikuhujumu uchumi kutokana na visa vyao vya ufisadi dhidi ya wachuuzi hawa," alisema Awiti.

Akizungumza baada ya kikao na Mahakama Kuu jijini Mombasa kuhusiana na tatizo hilo, Awiti aliitaka serikali kuu kulitilia maanani swala hilo, na kulipa kipao mbele.

"Kama Rais Uhuru Kenyatta alisafiri hadi Somalia ili kutatua marufuku ya miraa iliyokuwa imewekwa na serikali hiyo dhidi ya ndugu zetu kutoka Meru, mbona isiwe kama hivyo kwa ndugu zetu Wamijikenda? Tunamuomba Rais aingilie kati swala hili na ikiwezekana afungue kiwanda kitakachoweza kusafirisha mnazi hadi chi za nje,” alisema Awiti.