Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kujenga vibanda kwa wachuuzi wa mji wa Kisii ili kuendesha biashara zao siku zima bila kushuhudia changamoto wanapofanya biashara zao.
Ombi hilo linatolewa baada ya wachuuzi hao kusema kuwa wakati mvua inayesha huwalazimu kufungasha biashara na wanapoenda katika maduka y wafanyibiashara wenza ili kujistiri kutokana na mvua wao hufukuzwa hivyo basi wanaomba serikali kuwajengea vibanda watakapolipa ushuru kila siku.
Wakizungumza nasi mnamo mjini Kisii wachuuzi hao wakiongozwa na Jane Mong’ina na Evans Bina walisema huwa wanapitia wakati mgumu katika kuendesha biashara zao.
“Serikali ya kaunti ilijengea waendeshaji pikipiki vibanda na wanajikinga wakati wa mvua na wakati wa jua kali mbona sisi tusijengewe kama wao, tunaomba serikali kutujengea ili kujali maslahi yetu,” alisema Mong’ina.
Kila mfanyibiashara analipa ushuru ata sisi wenyewe tunalipa ushuru mbona tunatengwa kwa wakati huu wote, tunaomba serikali kutujengea vibanda ikiwa wanahitaji kutenda haki kwa wote,” alisema Bina.