Wachuuzi katika viungani mwa Kibera wametizia kuandamana kwa kile wanachosema kuwa kuhangaishwa na maafisa wa ukusanyaji uzulu na wale wa kaunti.
Wachuuzi hao wakiongozwa na naibu mwenyekiti wao, Joshua Kebati katika soko la Laini Saba viungani mwa Kibera, wachuuzi hao walilalamika kuangaishwa kila wanapofanya baishara zao katika Kibera.
"Hivi karibuni, iwapo maafisa wa ukusanyaji uzulu hawatabadilisha tabia zao na kukoma kutuangaiza tutaandama mpaka, afisi ya gavana kueleza shida zetu,’’ alinena Kebati.
Aidha Ken Mutinda ambaye pia ni mchuuzi aliongeza kuwa ni haki kwa kila mchuuzi kufanya biashara yake ndani ya Kibera bila ubaguzi ili kuendelesha ukuaji wa uchumi nchini.
"Maafisa wa baraza la kaunti ya Nairobi wanapaswa kuheshimu wachuuzi kama wafanyi biashara wengine ambao wamejitolea kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi umeimalika," alisema Mutinda.
Zaidi ya wachuuzi 200 wametiza kufanya maandamano ili kuwasilisha malalamizi yao kwa serikali ya kaunti ya Nairobi.