Wakulima wa viazi katika Kaunti ya Nakuru wamehimizwa kukubali kwa kauli moja sheria mpya ya upakiaji wa viazi ambayo ilipitishwa na bunge la kaunti.
Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua akizungumza na wakulima wa zao hilo katika maeneo mbali mbali wilayani Kuresoi, amewahimiza kukubatia sheria hiyo ambayo inapendekeza viazi kupakiwa kwa kilo hamsini.
Mbugua amesema serikali yake itawekeza zaidi katika sekta ya kilimo huku akiuliza wakulima kuwekeza zaidi katika kilimo biashara.
Amesema serikali ya kaunti imeweka vizuizi kadhaa katika barabara ya Molo Olenguruone, Molo - Nakuru na Mau Narok - Nakuru ili kuwanasa wanaokiuka sheria hiyo ya upakiaji wa viazi.
Waziri wa kilimo katika kaunti hiyo Bw. Stanley Chepkwony amewauliza wakulima kushirikiana na mamlaka ya kaunti ili kutekeleza sheria hiyo.
Amesema wakulima wamekuwa wakikandamizwa na wanunuzi wa viazi kwa miaka mingi bila hatua kuchukuliwa na serikali.
Aidha wale watakao kiuka sheria hiyo watapigwa fani ya Sh 500,000 ama wahudumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani ama vote viwili.