Wafanyi biashara wa mbao wamewaomba magavana kutojihusisha na maswala ya misitu kwani wanataka kusimamia misitu hiyo.
Wafanyi biashara wa hao walisimama kidete kusema kuwa wangependa misitu ishughulikiwe na serikali kuu wala si serikali za kaunti kwani wana matumaini kuwa serikali kuu ina uwezo na raslimali za kutosha.
Vile vile waliishukuru serikali kwa kutoa marufuku iliyokuwa imeweka haya yalisemwa na askofu Joel Songok ambaye ni mwenyekiti wa wafanyibiashara wa mbao katika eneo la North Rift.
Akihutubia vyombo vya habari hii leo, alimwomba bwana Tolgos kutowajumuisha pamoja hasa kwa tofauti ya Embobut ni kuwa serikali inaangalia hayo.
Aidha alisema kuwa misitu imewasaidia vijana kupata ajira na kuwa iwapo misitu itasimamishwa, vijana wataandikwa na akina nani alisema na waomba serikali ya kaunti kuwaajiri waliobobea katika maswala ya miti na siye kila yeyote ambaye anadai kuwa miti inaharibiwa na hana ujuzi wa miti.
Kando na hayo aliongeza kuwa walikutana na mawaziri katika wizara ya mazingira wa kaunti na kuwa waliwateua watu kadhaa kutoa ripoti kamili ya misitu.
Wamezuru misitu katika kaunti mbali mbali ikiwemo Uasin Gishu, Nandi, Vihiga, keiyo, transnzoia na Bungoma na kuwa hakuna uharibifu wowote wa misitu na kuwa miti hukatwa kwa mpango kwani wao hupewa leseni ya kukata miti.