Mkuu wa Idara ya Utalii katika Kaunti ya Mombasa Binti Omar ametoa changamoto kwa wadau katika sekta ya utalii kuzingatia mbinu mpya za utalii ili kuinua sekta hiyo katika eneo la Pwani, na nchi nzima kwa jumla.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza na wanahabari katika hoteli moja jijini Mombasa siku ya Jumatano, Omar alisema licha ya kuwa sekta ya utalii imetoa ajira kwa takriban watu laki nne, asilimia 70 ya idadi hiyo hawana masomo maalum ya kuhudumia watalii vyema.

Binti alisema hilo ni jambo la kutia wasiwasi hasa ikizingatiwa kuwa sekta hiyo inashindana na nchi zingine katika kuvutia watalii.

Alitoa changamoto kwa Chuo cha Utalii na wadau wengine kuzidisha mafunzo kwa wanafunzi wake ili kuwa na mbinu mpya na bora za kuvutia watalii humu nchini.