Mwenyekiti wa Wanabodaboda katika kituo cha Rioma kilichoko lokesheni ya Mwamonari wadi ya Sensi kaunti ya Kisii Robert Monyenyi amemwomba mwakilishi wa wadi hiyo Ochong’a Nyagaka kutengeneza daranja lililoanguka ambalo lililoko eneo la Ngure.
Mwenyekiti huyo na wanabodaboda wengine walikiri kuwa daranja hilo la eneo la Ngure limeharibika, limeziba na halipitishi maji ambayo hujaa kwa barabara na kukwaza shughuli zao za biashara.
“Tunamwomba mwakilishi wetu Ochong’a Nyagaka kutengeneza daranja hili la Ngure maana shughuli za uchukuzi simesimama kwa majuma mawili yaliyopita,” alisema Robert Monyenyi.
“Mimi sifanyi biashara kwenda sehemu hiyo ya kuenda eneo la Botobori ingawaje sehemu hiyo ndio huwa na wateja wengi kwa upendo wake tunamwomba kwa unyenyekevu atukumbuke na kukarabati daranja hilo tunaofya sana ,” alihoji Wyclif Rosana mwanabodaboda.
Wakati huo huo, wanabodaboda hao walisema siku ya Alhamisi mwanabodaboda mwezao Evans Ondieki aliteleza na kuchukuliwa na maji pamoja na mteja wake lakini kwa bahati nzuri wakaokolewa na wasamalia wema na kunusurika kifo.
“Mmoja wetu angefariki wiki jana wakati maji yalijaa kwa daranja hilo la Rioma ambalo limearibika kubindukia tunaomba mwakilishi wetu aingilie kati na kutengeneza daraja hilo hiyo maana hawezi kusubiri mpaka mtu akufe harafu atengeneze daranja hilo,” aliongezea Robert Monyenyi.
Kwa upande mwingine wakaazi wa eneo la Getenga eneo lililoko karibu na daranja hilo walisema hata wao wanaofya kwani wanaeza chukuliwa na maji.
“Mwakilishi wetu atengeneze daranja hili la sivyo tutaandamana tumempatia wiki moja kutengeneza daranja hili kikamilifu,” aliagiza Elijah Onderi mkaazi.