Mwenyekiti wa vituo 30 vya wanendeshaji bodaboda katika mji wa Kisii Mice Mose amewaomba wanao endesha bodaboda kutoandamana jambo mbaya linapotokea katika mji wa Kisii.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na wanabodaboda hao siku na Jumapili katika kituo chao kilichoko eneo la Capital, Mji wa Kisii mwenyekiti huyo aliwaomba kutoandamana kwani waendeshaji bodaboda ndio wanalaumiwa kwanza.

“Nawaomba waendeshaji bodaboda wa Kisii mheshimu viongonzi wenu. Mambo ya kuandama si suluhisho. Wiki jana wanafunzi wa taasisi ya Gusii Institute of Technology walipoandamana, wengi walisema ni waendeshaji bodaboda waliokuwa wakizua rabsha,” alisema Mose.

Wakati huo huo, mwenyekiti huyo alisema kuwa mwishoni mwa mwezi huu watafanya uchagunzi wa kuchagua wasimamizi ambao watakua wanaripoti mahitaji ya kila kituo ili jibu halisi kutafutwa kwa lile wanahitaji kushugulikiwa.

“Kuna baadhi ya waendeshaji bodaboda nilipokezwa habari kuwa walienda katika soko la Daraja Mbili na wakachukuwa vitu vya mfanyibiashara mmoja. Nawaomba wajitokeze waje ofisini mwangu wakiwa na vitu hivyo ili mwenyewe arejeshewe la sivyo mtachukuliwa hatua maana mnajulikana,” aliongezea Mose.

Aidha, waendeshaji bodaboda wa kituo hicho walimwomba mwenyekiti wao kusukuma serikali ya kaunti ya Kisii kuwakumbuka na kuwajengea vibanda ambavyo vitawasaidia wakati wa mvua na hata wakati wa jua kali.

“Huwa tunasumbuka na jua kali na wakati mwingine mvua inatunyeshea.  Tunakuomba ujaribu uwezavyo kuhakikisha kuwa tumejengewa vibanda na serikal ya kaunti yetu maana tunalipa ushuru kila mwezi,” alisema Jackson Osante mwendeshaji bodaboda.