Waendeshaji bodaboda kutoka eneo la Ikonge, Wadi ya Ekerenyo eneo Bunge la Mugirango Magharibi katika Kaunti ya Nyamira wamewaomba maafisa wa usalama kuwasaka wezi wa pikipiki katika eneo hilo.
Wakiongea siku ya Jumapili katika soko la Ikonge, vijana hao walisema kuwa kuna genge la majambazi ambao wametokea katika eneo hilo na kuwaibia pikipiki. Kwa sasa wamewataka maafisa wa usalama kuweka usalama na kuwasaka wezi hao ili waweze kuchukuliwa hatua ya kisheria.
Vijana hao walisema kuwa kufuatia kuhangaishwa na genge hilo, biashara zimerudi chini kwa kuwa wanaogopa kufanya biashara haswa wakati wa jioni na usiku kwani wajambazi hao wanawategea wakati kama huo.
Kwa sasa wamewaomba wamewaomba waendeshaji bodaboda wenzao kuwa macho na kuripoti yeyote anayeshukiwa kuwa anatenda uhalifu huo katika sehemu hiyo akijifanya kuwa mwenzao.
“Nawaomba maafisa wetu wa usalama kuwekea usalama wa kutosha katika eneo hili na kuwasaka wezi hao kwa kuwa tunahoia maisha yetu," alihoji Markson Gichana, mwendeshaji bodaboda.
Pia walisema kuwa wengine wao wamepoteza kazi kwani wenye pikipiki wameogopa kuwa uenda pikipiki zao zikaibiwa.
“Wengi wetu wamepoteza kazi kwani wamiliki wa pikipiki wamezichukua kwa kuhofia kuibiwa na wezi hao na hiyo imefanya vijana hao kukosa kazi,” alihoji Peterson Mogere, mwendesha bodaboda mwingine.