Wafanyabishara katika wadi ya Magwagwa wamejengewa kibanda watachokuwa wakitumia kufanyia biashara zao. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanya biashara hao katika soko la Magwagwa wanafurahia kazi ya mwakilishi wao wa wadi kwa kushirikiana na serikali ya kaunti na kuwajengea kibanda hicho.

Haya yanajiri baada ya wafanyabiashara hao kuendeleza biashara zao katika vibanda mbovu kwa muda mrefu uliopita. 

"Tumefurahia sana kwa kazi nzuri mwakilishi wa wadi yetu ambaye ametusaidia hasa sisi kama wanabiashara kwa kutujengea kibanda cha kufanyia biashara, na tunamwambia asante sana," alisema mfanyabiashara mmoja. 

"Wafanyabiashara katika soko hili wanapata shida nyingi kama wakati wa mvua na jua kali, hii inabidi kutatizika kwa biashara zao, ilibidi tukafanya mpango na serikali ya kaunti na kuamua kuwajengea wakazi hawa kibanda," alisema mwakilishi wadi Fred Nyachae.

Biashara katika soko hilo inatarajiwa kukua kwa kiasi kikubwa sasa.