Wanabiashara wa soko ya Mogonga liliyoko eneo bunge la Bomachoge borabu kaunti ya Kisii wamemwomba gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae kufanya maendeleo sawia na sehemu zote za kaunti hiyo
Wakiongea na mwandishi huyu hii leo katika soko hilo, wanabiashara hao waliomba gavana kujali maslahi yao kwa kukarabati soko hilo ambalo limeonekana kuwa changamoto kubwa zaidi kwani husumbuka sana na wanatozwa ushuru.
“Mvua inaponyesha tunasumbuka sana tunanunua bidhaa zetu kisha mvua inapokamilika kunyesha tunaaza kurudisha kwa soko tena na bidhaa zetu huchafuka sana na hiyo ni shida kwetu sisi wanabiashara,” alisema Jeruza Bitega, mwanabiashara.
Wakati huo huo, wanabiashara hao walisema wanahitaji kuona soko hilo kukarabatiwa sawa na soko zingine.
“Kila siku tunapofanya biashara hapa lazima tutozwe ushuru na hatujui hizo pesa zinaenda wapi, mbona pesa hizo zisitumike kujenga vibanda katika soko hii yetu,” aliuliza Gladys Osanse muuza nguo katika soko hilo.
Aidha, wanabiashara hao walikiri kuwa maji hupita katikati mwa soko hilo, na kuomba wawekewe mabomba ya kupitisha maji.
Sasa kibarua ni kwa serikali ya kaunti hiyo ya Kisii kujali maslahi ya wanabiashara hao baada ya wanabiashara hao kukiri kuwa wanatozwa ushuru ambao unaweza kutumika kujenga vibanda na kukarabati soko hilo kikamilifu.
“Sisi tumesubiri kupokezwa jibu halisi kutoka kwa serikali yetu baada ya kusumbuka kwa mda mrefu kuhusiana na ujenzi wa soko hili.,” aliongeza Osanse.