Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyabiashara wawili wamehukumiwa kifungo cha miezi miwili gerezani kwa kosa la kupatikana na mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku nchini.Francis Kyalo na Hassan Chalo ambao ni wachuuzi wa matunda walipatikana na mifuko hiyo iliyopigwa marufuku katika eneo la Sabasaba jijini Mombasa siku ya Jumatano.Washtakiwa hao walikubali mashtaka hayo mbele ya Hakimu Charles Ndegwa siku ya Alhamisi.Hakimu Ndegwa aliagiza wawili hao kufungwa kifungo cha miezi miwili jela ama walipe faini ya shilingi elfu tano kila mmoja.Akitoa uamuzi huo, Hakimu Ndegwa alisema hatua hiyo itakuwa funzo kwa wale ambao wanaendeleza utumizi wa mifuko hiyo ya plastiki licha ya kupigwa marufuku.Haya yanajiri baada ya wafanyabiashara wengine 11 kuachiliwa huru siku ya Jumanne baada ya kushtakiwa kwa makosa sawia na hayo.