Mahakama kuu jjijini Mombasa imekubali ombi la kulipwa kwa wafanyabiashara waliowekeza katika Benki ya Imperial.
Mahakama hiyo imeondoa agizo lake la hapo awali la kusitisha malipo hayo.
Haya yanajiiri baada ya mfanyabiashara Ashok Dosh kutaka Benki kuu na Benki ya Imperial kufanya kikao cha maridhiano ya jinsi ya kulipwa pesa zao.
Jaji Patrick Otieno aliondoa kikwazo hicho baada ya kukamilika kwa maridhiano hayo siku ya Ijumaa, ndani ya jengo la mahakama.
Mwezi wa Aprili mwaka huu, Mahakama ilisisitisha ulipaji wa pesa hizo baada ya mfanyabiashara mashuhuri jijini Mombasa Ashok Doshi, kuwasilisha ombi hilo mbele ya mahakama.
Doshi amewekeza shilingi bilioni moja katika benki hiyo.
Benki ya Imperial ilifungwa mnamo Oktoba 13, mwaka jana.