Wafanyabiashara wa soko la Laini Saba wameiomba serikali ya kaunti ya Nairobi kuwapa maafisa wao vitambulisho maalumu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Vitambulisho hivi vitatumiwa kuwatambulisha maafisa hao mbali na kuvaa sare zao za kazi ambazo mtu yeyote anaeza kununua na kuvaa.

Wanabiashara hao wamedai kuwa kuna maafisa ambao hukusanya ushuru bila kujitambulisha wanapo ombwa kujitambulisha na wafanyabiashara, hali ambayo wanasema huwatia uoga wafanyabiashara ikizingatiwa kuwa kuna watu ambao hulaghai wafanyabiashara kwa kizingizio kuwa wao ni maafisa wa kukusanya ushuru kutoka kaunti ya Nairobi.

Akiongea siku ya Jumanne katika soko la Laini Saba, Bonface Onchego mfanyabiashara alisema kuwa itakuwa rahisi kwa wengi wa wafanyabiashara wanaohudumu si tu kwenye soko hilo bali masoko yote yaliyo kwenye kaunti ya Nairobi kuweza kutambua ni nani afisaa halali. Aidha, Onchego alifafanua umuhimu wa kuwa na vitambulisho hivyo na kusema itasaidia kaunti ya Nairobi haswa viungani mwa Kibera kukusanya ushuru kutoka kwa wafanyabiashara na kusaidia kuwapa wakaazi huduma za kuridhisha haswa katika ujenzi wa masoko yalioko ndani viumgani mwa Kibera.

“Hii pesa ambayo inakusanywa na matapeli na walaghai ambao wengine wao hatuwajui ingetumiwa kwenye maendeleo katika soko letu na naiomba serikali ya kaunti kuwapa mafisa wa kutoza ushuru vitambulisho maalumu ili iwe rahisi kuwatambua maafisa haramu na wale halali kwenye idara ya kukusanya ushuru kila siku kutoka kwetu sababu hatujui nani ndiye nani,” alisema Onchego.