Zaidi ya wafanyikazi 3,500 kutoka kampuni ya maua ya karuturi iliyoko mjini Naivasha sasa wametaka swala la umiliki wa kampuni hiyo kutatuliwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyikazi hao wamesema kuwa walikuwa kwenye giza na hawakufahamu kinachoendelea kufuatia agizo la mahakama kuwa kampuni hiyo iuzwe.

Katibu wa chama cha wafanyikazi hao tawi la Naivasha Ferdinand Juma amesema kuwa hali ya sasa ya kampuni hiyo sio njema kwani hakuna anayejua hatua itakayochukuliwa baada ya kampuni hiyo kuuzwa.

"Wafanyikazi wengi wamefanya kazi katika eneo hili kwa zaidi ya miaka ishirini na hatma yao haijulikani. Tungependa swala hili litatuliwe mara moja," alisema Bw Juma.

Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mfanyabiashara Antony Rebo wamesema kuwa hatua ya kuuzwa kwa kampuni hiyo itaadhiri pakubwa uchumi wa mji huo huku maelfu ya kazi zikipotezwa.

"Hatma yetu haijulikani kwa kuwa ikiwa kampuni hii itauzwa, basi hatuna la ziada ila nasi pia kupigwa kalamu kwa kuwa tutakuwa tumepoteza kazi," alisema Bw Rebo.