Mahakama ya Mombasa imewaachilia kwa dhamana ya shilingi laki tatu wafanyikazi 13 wa Bandari ya Mombasa KPA, na halmashauri ya utozaji ushuru nchini KRA.

Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa hao wanakabiliwa na mashtaka ya utumizi mbaya wa afisi.

Abdi Mohamed Ali na wengine wanadaiwa kufanikisha utoaji wa makasha matutu kinyume cha sharia, ambapo pia walisababisha hasara ya shilingi milioni tisa.

Wafanyakazi hao wanadaiwa kushirikiana na mabwenyeynye kukwepa ulipaji ushuru wa shilingi milioni 9.

Mahakama pia imewatoza dhamana ya shilingi laki moja pesa taslimu iwapo watashindwa kulipa dhamana ya shilingi laki tatu.

Maafisa hao walikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Daglous Ogoti siku ya Ijumaa.

Kesi hiyo itasikizwa Septemba 13, mwaka huu.