Jengo la Mahakama ya Mombasa.[Picha/ the-star.co.ke]
Wafanyakazi watatu wa kampuni ya Coast Bus wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa siku ya Jumatatu.Watatu hao, Qainay Abubakar, Fatuma Muhadham na Athuman Mwakimako wanakabiliwa na shtaka la kuhudumu bila kibali.Washukiwa hao wanadaiwa kutoa huduma za posta pasi kibali mwafaka.Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa watatu hao walipatikana wakitoa huduma za posta pasi kibali kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini.Wafanyakazi hao wa Coast Bus wanadaiwa kutekeleza kosa hilo mnamo Desemba 1, 2017 katika kampuni ya Coast Mail Ltd iliyoko jijini Mombasa.Hata hivyo, washukiwa hao walikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Martin Rebera.Hakimu Rebera ameagiza watatu hao kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 10,000 pesa taslimu kila mmoja.