Wafanyikazi wa idara mbali mbali za serikali na za kibinafsi wanaotoka nje ya kaunti ya Mandera na wanaohudumu katika kaunti hiyo wanaendelea kuhama kutoka eneo hilo wakihofia usalama wao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na mfanyibiashara mmoja kwa jina John Kimani, ambaye aliwasiri Nakuru siku ya Alhamisi, biashara imekuwa tatizo kuu hasa wakati usalama umekuwa tishio kwa wenyeji wasiokuwa wa dini ya kiislamu.

Kimani amehoji kuwa, walilazimika kulala katika kituo cha polisi huku wakiyaacha mali yao mikononi mwa adui wao.

Katika uwanja wa ndege wa Mandera na vituo vya magari, wakenya wamefurika katika eneo hilo wakiwa wamebeba mizigo yao tayari kuhama kaunti hiyo.

Wafanyikazi hao wakiongea na waandishi wa habari wamesema kuwa watarudi katika kaunti hiyo pale serikali itakapo wahakikishia usalama .

Tume ya kuwaajiri waalimu na ile ya wahudumu hospitalini imewarai wanachama wao kusitisha kutoa huduma zao na kurejea makwao huku ikiwaomba watafute kazi mahala mbadala, ambamo mna usalama dhabiti.

Gavana wa kaunti hiyo Ali Roba amesema kuwa visa vinavyotokea katika kaunti hiyo vinaathiri mno uchumi wa kaunti hiyo, na akaitaka serikali kuboresha usalama ili kuvutia waekezaji.