[Picha/thestar.co.ke]
Wafanyibiashara katika wanaoendeleza biashara zao katika soko la Kongowea wametakiwa kutolipa kodi mpaka pale watakapo pata huduma bora katika soko hilo.
Akiwahutubia wakaazi wa Mombasa katika majengo ya soko hilo siku ya jumatatu hilo Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa hataruhusu kamwe kuona wananchi wananyanyaswa .
Uhuru hata hivyo ameongezea kuwa yeyeto atakayepatikana akiwalipisha kodi wafanyibiashara katika soko hilo watachukuliwa hatua za kisheria.
Kiongozi wa nchi aidha amemtaka mshirikishi wa utawala ukanda wa pwani kukabiliana na watoza ushuru bandia katika soko hilo la sivyo apigwe kalamu.
Hata hivyo ameahidi kwamba vijana wa mradi kwa vijana, NYS, watasafisha soko hilo ili kuona kwamba wafanyibiashara wanapata mazingira bora kwenye biashara zao.
Rais aliwapiga marufuku askari wa kaunti ya mombasa kukukusanya ushuru wa soko hilo kwa sababu huduma ni mbovu.