Wafanyibiashara katika soko la Kenyatta wameombwa kujiunga katika vikundi mbalimbali ili waweze kujiendeleza katika biashara zao.
Ombi hilo limetolewa na Catherine Ouma, ambaye pia ni mfanyibiashara katika soko hilo.
Akiongea Ijumaa, katika soko hilo Bi. Ouma alisema kuwa iwapo wafanyibiashara wadogo watajiunga na kujiandikisha katika makundi mbalimbali kuna uwezo wa kuendelea zaidi katika biashara zao.
“Kama wafanyibiashara tunafaa kuwa na vikundi kadhaa iwapo tukitaka kuchukua mkopo kutoka kwa benki itakuwa rahisi na hii itatuwezesha kama wafanyibiashara kujiendeleza,’’ alisema Bi. Ouma.
Mfanyibiashara huyo alieleleza kuwa kabla anze baishara ya kuuza mboga na nyanya alilazimika kuchukua mkopo kutoka kwa kikundi ili aanze.
“Kama wafanyibiashara tunahitaji pesa za kuinua biashara zetu. Siku hizi benki zimepunguza riba inayolipwa wakati mikopo imeombwa na hii itasaidia wafanyibiashara kuwekeza katika biashara”, alimalizia Bi. Ouma.