Wafanyikazi katika bandari ya Mombasa wanaopitisha mizigo zilizoletwa humu nchini wamelalamikia kukosekana kwa bidhaa za kupitishwa wakisema kuwa uhaba huo umesababishwa nakutozwa ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoletwa.
Mwenyekiti wa muungano wao Bwana William Ojonyo amesema kuwa licha ya kuandaa mikutano mengi na maafisa kutoka bandarini wakitaka hali hiyo kuchunguzwa hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa na mamlaka ya utozaji ushuru nchini KRA.
Ojoyo amesema kuwa huenda hali hiyo ikaathiri biashara nchini kwa kuwa washikadau wengi katika sekta hiyo huenda wakaanza kutumia bandari ya nchi jirani Tanzania katika kuleta bidhaa zao.
Hata hivyo wafanyikazi hao wamesema kuwa wana imani huenda hali nzuri ya kibiashara itarejea bandarini humo iwapo maafisa wa mamlaka hiyo pamoja na wale kutoka katika wizara ya fedha watakubali ombi lao ambalo wamewasilisha wakitaka ushuru unaotozwa kulainishwa.