Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wafanyibiashara katika soko la Keumbu, Kaunti ya Kisii wameipongeza serikali ya kaunti yao kwa kuweka kikundi cha vijana wanaofagia soko hilo.

Wakiongea katika soko hilo siku ya Jamatatu ilioko eneo bunge la Nyaribara Chache, wafanyibiashara hao walisema soko hilo limekuwa safi sana bila kero la taka.

“Napongeza seriakli ya Kaunti ya Kisii kwa vijana hawa wanaofanya usafi katika mji huu maanake siku hizi soko hili ni safi kila kuchao. Nwaapongeza vijana hawa pia kwa kazi nzuri wanaofanya ya kujitolea ili mji wetu uendelea kuwa msafi,” alihoji Truphena Makini, mfanyibiashara.

Aidha, walisema kuwa uwepo wa vijana hao ni njia moja yao kupata kazi ya kujiendeleza kimaisha na kuomba serikali iweze kuwaajiri vijana wengine zaidi kama njia mojawapo ya  kujiendeleza kimaisha.

Wafanyibiashara hao pia wamewaomba wenzao kutotupa taka mahali popote kurahisisha kazi ya vijana hao wakiongeza kuwa usafi ni muhimu kwa kila mtu.

Kwa upande wa kituo cha magari ambacho kinaendelea kukarabatiwa, walisema kitawasaidia pakubwa kwa kuwa gari zitakuwa na mahali pakubebea wasafiri ambao walisema wataweza kununua kutoka kwao.

“Nitumaini kuwa kituo hiki kikikamili biashara zetu zitanawiri kwani tutakuwa na watu wengi wa kununua bidhaa zetu wakisubiri gari," alihoji Hezron Masara, mfanyibiashra wa ndizi.