Wafanyibiashara katika soko la Ikonge kaunti ya Nyamira wameiomba serikali yao kuwanjengea Vyoo.
Wakiongea siku ya Jumanne asubuhi katika soko hilo wanabiashara hao wameiomba serikali ya Nyamira kuwajengea vyoo kwa kuwa wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu.
“Tumekuwa tukisumbuka sana hasa siku za soko kwa kuwa hatuna mahali pakujisaidia,” akasema Peter Kebaso mwanabiashara.
Kulingana na wafanyi biashara hao soko la Ikonge ni moja ya masoko makubwa katika kaunti ya Nyamira na hujumuisha wanabiashara kutoka kaunti zingine kama vile kaunti ya Kisii, Migori miongoni mwa nyinginezo.
“Gavana wetu anapaswa kujua kuwa usafi ni swala muhimu sana hasa mahali kama hapa ambapo tunauza chakula,” akasema Gladys Kiage mwanabiashara.
Kiage anaendelea kuwa ni swala la aibu kuwa soko kama hilo halina mahali pa kujisaidia ilhali huletea kaunti hiyo pesa kupitia ushuru.
Kwa sasa wanabiashara hao wamekuwa wakitumia vyoo vya majirani.