Maafisa wa polisi wilayani Marani eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini wameombwa kufanya msako na kuwatia mbaroni wezi wanaoiba bidhaa vya wafanyibiashara wa jua kali mjini Marani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wito huo umetolewa baada ya wafanyibiashara hao wa jua kali kuibiwa bidhaa vya vyuma mbalimbali ambavyo walisema vinawagharimu pesa nyingi.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne mjini Marani, wafanyibiashara hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Jackson Onderi, walisema kuwa baadhi ya washukiwa wa wizi huwa wanaiba vyuma vyao kutoka mahala wanapotengenezea bidhaa zao hasa wakati wa usiku.

Wafanyibiashara hao walisema wao huacha bidhaa hivyo nje kwani ni vingi na kuwataka maafisa wa polisi kuwasaka na kuwatia mbaroni wezi hao.

Onderi alisema vifaa vilivyoibiwa ni vyuma vya kutengeneza jiko, sanduku, miongoni mwa bidhaa zingine.

“Tunaomba maafisa wa polisi kuwasaka watu hao na kuwachukulia hatua kali kwani wamekuwa na mazoea ya kutuibia kila wakati hasa wakati wa usiku,” alisema Onderi.

Wakati huo huo, wafanybiashara hao wamewaonya wanaofanya kazi ya kukusanya vifaa vya chuma malighafi katika mji huo kwa kusema huenda wakachangia kwa vyuma vyao kupotea.

Walisema kuwa yeyote atakayepatikana na chuma katika mji huo anapaswa kuchukuliwa hatua kali ya kisheria kwani atashukiwa kuwa mmoja wa wezi hao.