Wafanyibiashara katika soko la Daraja Mbili mjini Kisii wameipongeza serikali ya kaunti kwa kujenga vyoo katika soko hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongea jana na mwadishi huyu katika soko la Daraja Mbili wafanybiashara hao walimpongeza gavana wa eneo hilo.

“Tunaipongeza Serikali ya kaunti ya Kisii kwa kutukumbuka na kutujengea vyoo katika soko hili letu kwa kuwa hiyo ni njia moja ya kudumisha usafi,” alisema James Kekere, mfanyibiashara.

Wafanyibiashara hao wamesema kuwa wamefaidika pakubwa na serikali za ugatuzi kwa kuwa ujenzi wa soko hilo umendelezwa na serikali ya kaunti ya Kisii imeweka mataa katika maeneo hayo.

“Kupitia kwa serikali za ugatuzi sisi kama wafanyibiashara tumeona mabadiliko makubwa katika soko letu na tunaomba serikali yetu ya kaunti kuendelea kutusaidia ili tuendelee kunawiri katika biashara zetu,”alisema Grace Kwamboka, mfanyibiashara.

Wafanyibiashara hao wameiomba wizara inayosimamia mazingira kuwa katika mstari wa mbele kukabiliana na wale wanaochafua soko hilo ili kufanya soko hili kuwa safi kila kuchao.

“Tunaomba Wizara ya Mazingira kuwachukulia hatua ya kisheria watu wale wanaochafua soko hili na kutupa uchafu kiholelaholela kwa kuwa mahali pabiashara panastahili kuwa pasafi,” alisema Samson Okindo, mfanyibiashara.

Ujenzi wa vyoo ni moja ya miradi ya serikali ya kaunti ya Kisii inayoongozwa na Gavana James Ongwae ili kuhakikisha kuwa soko la Daraja Mbili limekuwa la kisasa.