Wafanyibiashara katika soko la Laini Saba viungani mwa Kibera wamelalamikia wahudumu wa magari wanaoegesha magari yao kandokando mwa barabara katika soko.
Wafanyibiashara hao wanasema kuwa wateja wao huzuia kununua bidhaa zao kwa sababu wahudumu hao husababisha msongamano.
Wakiongea asubuhi ya Juymatatu katika soko hilo, wafanyibiashara walisema kuwa magari hayakubaliwi kuegeshwa katika soko hilo kwa sababu hakuna kituo cha kubebea abiria hapo na waliwalaumu maafisa wa polisi viungani mwa Kibera wanaokubalia magari kuegeshwa mahali ambapo hakuna kituo cha abiria. Aidha, wafanyibiashara hao walisema kuwa maafisa wa polisi upewa hongo na wahudumu hao ili kuruhusu magari kuegeshwa na hii inasababisha hasara kubwa kwa biashara yao kila siku.
Mmoja wa wafanyibiashara hao, Ann Nyaguta alisema kuwa wamekadhiria hasara kubwa kutokana na uegeshaji magari pahali ambapo wanafanyia biashara zao na wameomba shirika la uchunguzi wa magari kushughulikia suala hilo ili kukomesha hasara kutokana na msongamano ambao umechangia wateja kuzuzia kununua bidhaa zao.