Wafanyibiashara wa soko la Keroka wamelalamikia kutozwa ushuru mara mbili kwa siku na kusema wanaendelea kupata hasara kubwa kila wakati.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyibiashara hao wanatozwa ushuru na maafisa wa serikali ya kaunti ya Nyamira na wale wa kaunti ya Kisii na kupelekea kupata hasara kubwa, hayo ni kwa mujibu wa wafanyibiashara hao.

Wakizungumza mjini Keroka wakiongozwa na Mwakilishi wa wadi ya Rigoma kaunti ya Nyamira Benson Sironga, waliomba serikali hizo za Kisii na Nyamira kuelewana ili kutowatoza ushuru mara mbili kwa siku kwani nao wanasaka riziki.

“Wafanyibiashara wa soko la Keroka wamechoka kutozwa ushuru mara mbili kwa siku naomba maafisa wa kukusanya ushuru kuwa, wakati mfanyibiashara anakuonyesha risiti la ushuru hakuna haja ya kumtoza ushuru tena,” alisema Sironga.

Sironga alisema Mzozo ulioko katika mji wa Keroka ndio umepelekea hayo kuendelea huku akiomba magavana wa Kisii James Ongwae na wa Nyamira John Nyagarama kuja pamoja na viongozi wengine kuokoa wafanyibiashara.