Zaidi ya wafanyikazi 2,600 kutoka kampuni ya maua ya Karuturi sasa wamefukuzwa nyumbani baada ya kampuni hiyo kufungwa.
Aidha maisha ya wafanyikazi hao kutoka kampuni hiyo haijulikani kufuatia kufungwa huko kulikoagizwa na mahakama moja mapema mwezi jana.
Aidha usimamizi wa muda wa kampuni hiyo aidha umewataka wafanyikazi hao kuondoka katika Nyumba zinazomilikuwa na Karuturi katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
Sasa haijulikani bayana hatma ya kampuni hiyo, shule ya msingi, ya upili ambazo zaidi ya watoto 2,000 wanasomea pamoja na hospitali iliyokuwa ikiongoza eneo hilo.
Msimamizi mkuu wa maswala ya leba wilayani Naivasha Moses Karimi amedhibitisha kufungwa huko na kusema kuwa wafanyikazi hao watalipwa mishahara ya mwezi wa aprili.
"Wafanyikazi hawa watalipwa mshahara wa mwezi mwingine mmoja na leo Ijumaa, ni siku yao ya mwisho kuwa kazini," aliongeza Karimi.