Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Maji ni uhai. Utunzi wa mito ni jukumu la kila mkenya awe mdogo au mkubwa. 

Maisha ya kila kiumbe kilicho na uhai hutegemea maji kila uchao. Kila mara katika mitandao, hafla mbalimbali na hata vyombo vya habari, wimbo ni mmoja tuyatunze mazingira. 

Lakini kuna wale wameyatia masikio yao nta hawasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini.

Kulingana kijana mmoja aliyefumaniwa akitupa takataka katika mtoni katika eneo la Daraja Mbili, yeye alipewa takataka hizo na mfanyakazi mmoja wa kaunti anayelisafisha soko la Daraja Mbili. 

Mfanyabiashara mmoja anayefanya biashara karibu na mto huo ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa imekuwa mazoea yao kumwaga taka katika mto huo.

"Hawa watu wa kaunti wanaofagia sijui wanafikiria aje, wanawachukua machokoraa hawa wadogo wanawapa takakata na rukwama ili waje wazimwage hapa mtoni. Hata hii anayomwaga ni ile wamefagia tu hapo saa hii," alisema mfanyibiashara huyo.

"Badala ya kuweka pamoja ikauke wachome wanamwaga tu mtoni. Na sio mara ya kwanza huwa wanafanya hivyo," aliongeza kusema.

"Ukiangalia hii takataka iko na karatasi za nylon, nywele za watu na wanamwaga mtoni na kuna watu ambao wanatumia haya maji kwa mifugo au kazi zingine si hii ni kuletea watu magonjwa,” alifoka kwa uchungu mwanabiashara huyo.