Rais Uhuru Kenyatta sasa ameagiza wizara ya fedha kuondoa mara moja ushuru unaotozwa malipo ya ziada maarufu 'Overtime' na yale ya uzeeni kwa wafanyikazi wa mishahara ya chini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Rais alisema kuwa hatua hiyo inanuia kuwainua wakenya wenye mapato ya chini ili kuweza kuinua maisha yao kiuchumi.

Rais Kenyatta ameyasema haya baada ya kufungua rasmi warsha ya muungano wa waajiri nchini FKE katika hoteli ya Enashipai mjini Naivasha ambao umewaleta pamoja wajumbe kutoka mataifa 15 ya afrika.

Akihutumia kongamano hilo Ijumaa, Rais Kenyatta alisema: “Ukosefu wa kazi ni changamoto kubwa barani afrika na asilimia 70 haswa vijana  hawana ajira.”

Naye msimamizi mkuu wa shirika la International Labor Organization (ILO) nchini Chapinga Chuma amesema Afrika inakabiliwa na changamoto za miundo msingi.

Wengine waliozungumza ni pamoja na mwenyekiti wa muungano wa waajiri Linus Gitahi pamoja na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mivinyo ya Keroche Bi Tabitha Karanja.