Wafanyikazi na wauzaji wa bidhaa katika maduka ya jumla ya uchumi Mjini Nakuru, Wamelalamikia hatua ya kufunguwa kwa tawi la duka hilo mapema Jumatatu mjini humo bila ya kuwepo kwa ilani yoyote.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baadhi ya waliozungumza na wanahabari wakitaka majina yao kubanwa, wamesema vijana wengi watakosa ajira na wameitaka serikali kuhakikisha waliochangia kufungwa kwa maduka hayo wanafunguliwa mashtaka mara moja.

“Kuna wale ambao walikua uchumi na hawajachukuliwa hatua yoyote, watu kama sisai ambao tunasambaza bidhaa katika maduka haya tutafanya nini? Maduka yote ya uchumi katika miji tofauti yamefungwa, hebu fikiria ni watu ngapi wamepteza kazi!” muuzaji mmoja ambaye hakutaka kutajwa aliteta.

“Sisi kama vijana tunaumia kila wakati, sasa kufungwa kwa maduka haya ni kutunyanganya kazi,” aliongeza

Mkurugenzi mkuu wa maduka ya Uchumi Bw Julius Kipng’etich, Jumatatu alisema alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama ya kutoa huduma ili kuangazia miundo ya kisasa ya kibiashara.

Maduka mengine yaliyofungwa ni matawi ya Eldoret, Meru, Taj mall, Embu, Kisii na Kericho.

Kutokana na kufungwa kwa matawi hayo, wafanyakazi wapatao 253 wamepoteza kazi baada ya nafasi walizokuwa wakishikilia zikifutiliwa mbali.