Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa Nakuru Magharibi Samwel Arama ameshtumiwa na wafuasi wa CORD kutoka eneo hilo, kwa madai ya kuwa kibaraka cha mrengo unaoongoza Jubilee, haswa kufuatia msimamo wake wa sakata ya Eurobond.

Wakiongea mjini Nakuru wakiongozwa na Shem Osiako na Peter Otwori wote kutoka eneo bunge lake, wafuasi hao wa CORD walimlaumu Arama wakidai anakumbatia ufisadi kuliko kuukemea, na badaaye kuelekeza lawama kwa kinara wao Raila Odinga.

Hata hivyo, wamemtaka Arama kujiuzulu kutoka chama chao na kujiunga na Jubilee, wakisema ‘alinufaika na mradi wa ufisadi chini ya aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru’.

“Namuonya Samwel Arama atuheshimu na aheshimu CORD kwa jumla, kwa sababu pahali tunaelekea sasa hatufanyi siasa za hapa chini, tunataka siasa za kuangalia pahali pesa zetu zinaenda,” alisema Peter Otwori.

Wikendi iliyopita, Arama alimtaka Raila kuweka bayana anayoyaelewa kuhusu sakata hiyo ya Eurobond.