Waufasi wa mrengo pinzani wa Cord katika Kaunti ya Mombasa wametaka safari za raisi na naibu wake kupunguzwa ili kuepuka utumizi mbaya wa fedha za umma.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatano, wafuasi hao, wakiongozwa na Otieno Odhour, walisema kuwa wawili hao wanatumia pesa za umma vibaya hasa katika safari za nje.

Aidha, wakaazi hao walipendekeza wawili hao kutumia pesa zao za kibinafsi ili kuonyesha uzalendo wao kwa taifa na wananchi.

Hatua hii inajiri baada ya waziri wa fedha Henry Rotich, kusema gharama za usafiri za Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, zimeongezeka maradufu ikilinganishwa na za serikali zilizopita.

Kutokana na hilo, Rotich ameitaka kamati ya bajeti kuidhinisha shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya safari za wawili hao humu nchini.

Akiielezea kamati ya maswala ya bajeti jinsi shilingi bilioni 18 za fedha za ziada zilivyotumika, Rotich alisema shilingi bilioni 1.25 zilitumika kumlipa mmiliki wa Shamba la Waitiki Evans Waitiki.

Waziri huyo alisema fedha hizo zilitumika kutokana na matumizi ambayo hayajapangwa ambapo tayari Rais Uhuru atakuwa a na safari nyengine katika kaunti ya Nakuru, Nyandarua na Kiambu.