Mgombea wa kiti cha ubunge Mvita Omar Shalo akiwa na Rais Uhuru Kenyatta katika hafla ya awali. [Picha: Omar Shalo/ facebook.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wafuasi wa mgombea kiti cha ubunge Mvita Omar Shalo wametishia kutounga mkono chama cha Jubilee katika uchaguzi mkuu ujao iwapo Shalo hatapewa cheti cha chama hicho.Wafuasi hao wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kuhakikisha Shalo anakabidhiwa cheti cha ushindi ili aweze kugombea kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa Agosti.Wakiongozwa na Ahmed Mohammed, wafuasi hao walisema kuwa Shalo anapaswa kukabidhiwa cheti cha chama kwa kua yeye ndiye chaguo lao.“Sisi hatutaunga mkono Jubilee iwapo Shalo hatapewa cheti cha ushindi,” alisema Mohammed.Wafuasi hao walisema kuwa swala hilo lisipotatuliwa kwa haraka, watajiunga na chama chochote kile cha mrengo wa upinzani.“Tuko tayari kutafuta chama kingine tukiunge mkono iwapo Shallo hatapewa cheti,” aliongeza Mohammed.