Wafuasi wa NASA kutoka Mombasa wakiabiri basi siku ya Jumatatu kuelekea Nairobi kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Raila. [Picha/ nairobinews.nation.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulikuwa na kizaazaa siku ya Jumanne nje ya bunge la Kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa muungano wa NASA waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwa kinara wa mrengo huo wa upinzani Raila Odinga kukusanyika kudai marupurupu yao ya usafiri.Hii ni baada ya baadhi yao kuwalaumu wenzao kwa kutaka kulipwa licha ya kutohudhuria sherehe hizo zilizoandaliwa katika bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi siku ya Jumanne.Mwenyekiti wa kundi hilo ambaye hakutaka kutajwa, alidai kuwa kuna baadhi ya watu ambao walitumwa na serikali ya Jubilee kufuatilia mienendo ya waliohudhuria hafla hiyo.“Baadhi ya wafuasi hapa si wafuasi halisi wa NASA. Wametumwa tu na Jubilee ili kuharibu mipango yetu,” alidai.Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mfuasi sugu wa Gavana wa Mombasa Hassan Joho alisema kuwa walipitia mengi sana katika safari yao wakielekea Nairobi.“Baadhi ya watu ambao wanataka kulipwa hawawezi kutaja yaliyotendeka. Kunyanyaswa na polisi njiani, mateso ya kila aina na bado wanataka kulipwa,” aliongeza.Baadhi ya wahudumu wa bunge la Kaunti ya Mombasa walilazimika kuingilia kati ili kutuliza hali hiyo. Kuwa wa kwanza kujua kuhusiana na habari muhimu pindi zinapotokea. Tuma ujumbe kupitia nambari ya WhatsApp 0740950002 ukianza na mojawapo ya maneno yafuatayo ili uanze kupokea taarifa moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi: Mombasa Crime, Mombasa Politics, Mombasa Sports, Mombasa Agriculture, Mombasa Random, Mombasa Health, Mombasa Business, Mombasa Environment, Mombasa Entertainment, Mombasa Transport, Mombasa Opinion, Mombasa Education.