Sanduku la kura. [Picha/ theeastafrican.co.ke]
Baadhi ya wafuasi wa mrengo wa NASA Kaunti ya Kilifi wamesema kuwa hawatashiriki marudio ya uchaguzi wa urais.Wafuasi hao wameshinikiza kuahirishwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi hadi pale matakwa ya NASA yatakapozingatiwa.Wakiongozwa na mpiga kura Jamal Sheikh, wafuasi hao wamesema kuwa joto la kisiasa linaloshuhudiwa kwa sasa, ni ishara kuwa hakutafanyika uchaguzi wa haki na wazi.“Nchi imechafuka na joto la kisiasa limezidi hivyo sidhani kuwa uchaguzi utakuwa wa uwazi,” alisema Sheikh.Sheikh ameitaka Tume ya IEBC, kutoshinikizwa na Jubilee kusimamia uchaguzi huo wa Oktoba 26.“IEBC musikubali kutumiwa na Jubilee, fanyeni maamuzi yenu pasi ushawishi wa serikali,” alisema Sheikh siku ya Alhamisi.Aidha, Sheikh ametoa shinikizo la kujiuzulu kwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pamoja na baadhi ya makamishena wanaodaiwa kuchangia kuweko kwa dosari katika kura ya urais iliyofutiliwa mbali na Mahakama ya juu.Wakizungumza kwenye kikao na wanahabari mjini Malindi, wafuasi hao wa NASA walimpongeza Roselyn Akombe kwa kujiuzulu kama kamishena wa IEBC kwa kusema kuwa msimamo wake ni ishara ya uzalendo.