Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wafugaji kutoka kaunti ndogo ya Rongai wameonywa dhidi ya kuwachinja mifugo ambao wamefariki, kwani ni hatari kwa afya ya binadamu.

Akizungumza na mwandishi huyu Ijumaa, daktari mkuu wa mifugo eneo la Rongai Martin Karite alisema kwamba, wafugaji ambao wanaendeleza kitendo hicho wanajiweka kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa ambayo huambukizwa kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu.

"Nyama ya mifugo amabo wamekufa bila kujulikana kilichosababisha kukufa kwa mnyama huyo, bila shaka ni hatari kwa afya ya binadamu na nyama hiyo ndio wafugaji huuza na ningependa kuwaonya kuwa watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria," Karite alisema.

Aliongeza kuwa, mifugo wengi hufariki kutokana na magonjwa mbalimbali na wafugaji wanapaswa kuwa waangalifu.