Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa jimbo la Nakuru wameamua kubuni shirikisho ambalo litasaidia kujadili na viwanda vya maziwa kuhusu kustawisha bei ya ununuzi wa maziwa.
Wakulima wamelalamikia kugeuka kwa bei ya ununuzi wa maziwa.
Shirikisho la Nakuru County Dairy itaongozwa na James Ndung'u Karanja ambaye anamiliki Pokea Farm iliyoko kata Ndogo ya Njoro.
Atasaidiwa na wengine. Ingawa lengo kuu la shirikisho hili ni kupigania bei nzuri kwa wauzaji wa maziwa, ina mpango wa kubuni bodi kuu ambayo italeta wafugaji wa ng'ombe wa maziwa zaidi ya 500,000 na kupanua soko ya maziwa pamoja na kuwapa wakulima mikopo.
"Shirikisho hili litachangia kuongezeka kwa maziwa kwa sababu wakulima watayakusanya maziwa upande moja kabla ya kupelekwa viwandani," alisema Henry Ng'eno ambaye ni afisa was Nakuru County Dairy Value Chain.
Wakulima walikubaliana na mwelekeo huu katika mkutano uliofanyika wiki hii.