Waziri wa kilimo katika kaunti ya kisii Vincent sagwe amesema kiwanda cha samaki kitajengwa hivi karibuni katika kaunti ya kisii ili kuzuia kuooza kwa samaki wakati wanabiashara wanapoziuza na kuwasababishia hasara kubwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea siku ya Jumanne katika uwanja wa Nyamache katika kaunti ya Kisii kwa kampeni ya wakulima na wafugaji wa samaki, waziri alisema wizara yake imetenga pesa kwa wafugaji wa samaki ili waweze kujiendeleza na ufugaji huo bila shida yoyote kuwakumba.

Kampeni hiyo ya wafugaji inatarajiwa kufufua sekta hiyo ambayo kwa mda mrefu sasa imekuwa ikididimia katika eneo la kisii, ambapo wafugaji walipashwa kuendelea na ufugaji huo kwa motisha kwani una faida kubwa.

“Tukiwa na kiwanda cha samaki katika kauntii ya Kisii, nawahakikishia hamtakuawa na samaki ya kuuza katika masoko kama njia mojawapo ya  kuimarisha biashara ya samaki katika kaunti hii, sharti tuwe na kiwanda,” alisema Sagwe.

Aidha, waziri huyo aliwaomba wakulima na wafugaji kujiandikisha kwa chama cha Culture Association of Kenya, ili kupata afueni ya kupokea mafunzo ya ufugaji wa ambayo hutolewa na chama hicho bila malipo

“Nawaomba mjiandikishe nyinyi nyote kama wafugaji, maana ukiwa wewe peke yako bila kujiandikisha hautapata matunda ya mafunzo hayo kutoka kwa chama,” aliongezea sagwe.

Wakati huo huo, afisa mkuu wa sekta ya ufugaji katika kaunti ya kisii Samuel Nyakenyanya alisema changamoto ya kutopata mbegu ya samaki imefika kwani wanapania kuhakikisha shida hiyo inatatuliwa.