Wafungwa 221 katika magereza ya eneo la Pwani wataachiliwa huru kama hatua ya kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na wanahabari katika mahakama kuu ya Mombasa siku ya Jumanne, Jaji Luke Kimaru amesema kuwa hatua hii itasaidia kupunguza fedha zinazotumiwa na serikali kukidhi wafungwa wakiwa gerezani.

Ameongeza kuwa wafungwa watano wamepunguziwa kiwango cha hukumu yao, huku akiongeza kuwa kila mfungwa anaigharimu serikali shilingi mia mbili kila siku, hivyo basi kuitaja hatua hiyo inaongeza gharama kwa serikali.

Wafungwa hao wanatoka gereza la Shimo la Tewa, Kwale, Wundanyi na Voi.