Wagema 10 wilayani Nyamira kaunti ya Nyamira wametiwa mbaroni kwa kosa la kuendelea kutengeza pombe haramu ambayo ni kinyume na sheria nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea wakati wagema hao walikamatwa siku ya Jumanne, kamishena wa kaunti ya Nyamira Josephene Onunga alithibitisha kuwa waliwatia mbaroni wagema hao pamoja na kumwaga pombe pombe haramu lita 10,000 na chang’aa 1,000.

Kamishena Onunga aliomba wakazi Nyamira kujitenga na upikaji huo ambao ni kinuyume na sheria na kufanya biashara tofauti ili kujiendeleza.

“Upikaji pombe haramu haukubaliwi, fanyeni biashara tofauti kuendelea mbele badala ya kupika pombe,” alikiri Onunga.

Wakazi wa eneo la Nyamira walipongeza shughuli hiyo ya umwagaji pombe huku wengine wakisema pombe hiyo imeathiri watoto wao na ata wengine kuacha kuendelea na masomo.

“Tunaomba upikaji kukomeshwa na polisi wawe wanafanya msako wa kumwaga pombe kila wakati ili kusaidia vijana wetu ambao hutegemea pombe hiyo,” alihoji Beatrice Kerubo, mkaazi wa Nyamira.