Mwenyekiti wa chama cha kupambana na dawa za kulevya katika Kaunti ya Kisii Kasisi Lawrence Nyaanga amewahimiza waliokuwa wagema kukopa pesa kutoka hazina mbalimbali ikiwemo hazina ya Uwezo Fund ili kuanzisha biashara mbadala.
Alikuwa akiongea katika lokesheni ya Boronyi alipokutana na wagema 17 waliokukiri kuasi utayarishaji wa pombe haramu baada ya kukabiliana na maafisa wa polisi kwa mda mrefu.
Kasisi Nyaanga aliwahimiza waliokuwa wagema kutumia motisha ule walikuwa nayo hapo wali kufanya biashara tofauti na kukopa mikopo kuanzisha ukulima na biashara mbalimbali ili kujiendeleza
“Vile mumetangaza kuwa hamtapika pombe haramu tena nawahimiza muwe katika kikundi mkope pesa kutoka katika hazina zilioko ambazo ni za serikali na za mashirika mbalimbali ili muweze kujihusisha katika biashara tofauti kujikimu kimaisha,” alikiri Nyaanga.
"Naamini kuwa mkitumia ile motisha mlikuwa mnatumia katika upikaji pombe mtaendela mbele na kubadilisha maisha yenu,” aliongeza Nyaanga.