Wagombezi wa viti mbalimbali vya kisiasa katika kaunti ya Nyamira walipata wakati mgumu kupata nafasi ya kutangaza azma yao ya kupata viti hivyo kwenye matanga ya aliyekuwa mbunge wa Mugirango kaskazini Godfrey Masanya.
Mazishi hayo ambayo yalivutia maelfu ya waombolezaji na mamia ya wanasiasa kutoka sehemu mbalimbali humu nchini yaligeuka kuwa uwanja wa magombano kwani kila mwanasiasa alitaka kuhutubia umati huo ili angalau kutangaza nia yake ya kisiasa.
Aidha, waliopata nafasi kuzungumza walipigiwa kelele kwani inasemekana kila mwanasiasa alikuwa na wafuasi wake, jambo lililowapa wakati mgumu wapinzani kuzungumza.
Miongoni mwa wale walio pata nafasi ya kuzungumza kwa urahisi ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa utekeleezaji wa katiba Charles Nyachae na Mwenyekiti wa Jomo Kenyatta Foundation ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha ugavana katika kaunti hiyo Walter Nyambati.
Kwa wakati mwingine mmoja wa Mugirango kaskazini Charles Geni aliwarushia matusi waombolezaji hao alipopigiwa kelele.
Wabunge kama Joash Onyonka (kitutu chache), John Arama (Nakuru West) walilazimika kuondoka kabla ya kuzungumza waliposhindwa kukabiliana na joto la kelele kwenye mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na wanasiasa wengi.