Wakazi wa kaunti ya Nyamira wamepata nafuu baada ya serikali ya kaunti hiyo kuezeka mashine mpya ya kuosha damu kwa wagonjwa walioathirika na ugonjwa wa figo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama, kwa sasa wagonjwa wa figo ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta matibabu mbali na Nyamira wanaweza pata huduma hizo kwenye hospitali kuu ya Nyamira. 

"Wagonjwa wa figo ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta matibabu kwenye hospitali kuu ya Kenyatta na  hospitali ya mafunzo ya rufaa kule Eldoret wanaweza pata matibabu bora hapa Nyamira," alisema Nyagarama. 

Akizungumza katika kijiji cha Nyangoso kwenye eneo bunge la Mugirango magharibi siku ya Jumanne wiki hii, gavana Nyagarama alisema kuwa mashine  hiyo ambayo tayari imeezekwa kwenye hospitali ya Level Four ya Nyamira itawahudumia wakazi kwa bei nafuu. 

"Mashine ambayo imeezekwa kwenye hospitali ya Nyamira itawawezesha wagonjwa kupata huduma za matibabu kwa bei nafuu," alisema Nyagarama.