Afisa mhudumu wa Afya ya Jamii (community Clinical Officer) katika Kaunti ya Kisii Kepha King’oina amewasihi wakaazi wa Kisii kufuata maagizo ya Madaktari kuhusu kumeza dawa iwapo wamekumbwa na maradhi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa King’oina amewaambia wakaazi hao kutumia dawa vyema wanapougua ili kuepuka na kuendelea kuwa wagonjwa zaidi na kuambukiza wengine ugonjwa hasa walioko miongoni mwao.

Akiongea na Mwandishi wa Habari huyu Afisa King’oina alisema kuwa visa vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) imeongezeka katika jamii kutokana na watu wanaopimwa na kupatikana na ugonjwa huo ambao hupewa dawa na hawazitumii kulingana na masharti wanaopewa na madaktari.

“Mgonjwa ambaye ameathirika na ugonjwa wa kifua kikuu anastahili kunywa dawa kwa miezi sita ili apone kitu ambacho wagonjwa wengi hupuuza, kisa ambacho inapelekea kuzorota kwa afya yao,” alisema King’oina.

King’oina amesema wamemzuilia mgonjwa mmoja katika Hospitali ya Rufaa ya Kisii kutoka lokesheni ndogo ya Bonyamatuta Nyakoe eneo Bunge la Kitutu Chache Kusini, ambaye ameathrika zaidi na ugonjwa wa kifua kikuu kwa kukaidi kutumia dawa alizopewa na kwa sasa itabidi atumia dawa hizo kwa miezi minane ili apate nafuu.

“Wakati alipopewa dawa hizo hapo awali alizitumia kwa wiki tatu na kuacha kitu kilchochangia afya yake kuwa mbaya zaidi,” aliongezea King’oina.

Mgonjwa huyo kwa jina Alfred Maeba Amisi, inadaiwa amewaambukiza wenzake ugonjwa huo katika jamii alipokuwa nyumbani huku walioambukizwa wakiombwa kufika katika Hospitali ya Kisii ili kupewa ushauri na  mafunzo zaidi Kuhusu ugonjwa huo.

Vile vile, King’oina amesema kuwa watu wanapokua wagonjwa wameombwa kuachana na madawa za kulevya na kushughulikia afya yao kwanza kwa kuwa dawa na pombe haziambatani kamwe.

Aidha, king’oina amewashauri wanaofanya biashara za uchukuzi kutobeba watu wengi kupita kiasi kwa kuwa ni rahisi sana watu kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu wanapobanwa ndani ya gari ambayo mara nyingi hamna hewa safi na kupelekea asilimia kubwa ya watu kupata ugonjwa wa kifua kikuu.

“Magari hapa Kisii ubeba watu kupita kiasi na watu hubanwa bila kupata hewa safi na kuna uwezekano wakupata ugonjwa huu kama mmoja wao anao,” alidokeza King’oina.