p { margin-bottom: 0.08in; }

Share news tips with us here at Hivisasa

Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Garissa wamesema walipoteza stakabadhi muhimu wakati wa shambulizi chuoni humo wiki lililopita.

Kwa mujibu wa Walter K'Odipo ambaye pia ni katibu wa chama cha UASU tawi la Garissa, wengi wa wahadhiri walipoteza stakabadhi zao walipokuwa wakiokolewa na wanajeshi kutoka chuoni humo.

Katibu wa UASU Mugo K’Olale aidha ameitaka serikali kutoa taarifa kuhusu wanafunzi wa chuo cha Garissa kilichoshambuliwa na waasi wa Al-Shabaab juma lililopita na ambao hawajulikani waliko kufikia sasa.

Kulingana na K’Olale wanafunzi 152 waliuliwa katika shambulio hilo na wengine 166 hawajulikani waliko. Aidha kwa mujibu wa serikali, watu 147 waliuawa huku 79 wakijeruhiwa kwenye tukio hilo.

Anasema wanafunzi hao huenda walitekwa nyara na wanamgambo hao wa Al-Shabaab.

Haya yanajiri huku familia za waadhiriwa wa shambulizi hilo na ambao walizitambua maiti za wapendwa wao zikianza kuzichukua maiti hizo kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Chiromo.

Kufikia sasa miili ya watu 48 ambao walilazwa kwenye chumba hicho ndio bado haijajulikana.