Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki amewataka vijana waliojiunga na magenge ya kihalifu kujisalimisha mara moja kwa idara ya usalama.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Achoki alisema kuwa vijana hao watapewa usaidizi na ushauri na serikali kwa lengo la kuwatenga na uhalifu.

Akiwahutubia wanahabari siku ya Jumanne, Achoki alisema kwamba idara ya usalama imebaini kwamba baadhi ya vijana wamesajiliwa katika magenge hayo bila ya hiari yao.

“Ni vyema iwapo vijana hao watayaasi makundi hayo ya kijambazi na kutafuta usaidizi na ushauri kutoka kwa serikali,” alisema Achoki.

Hata hivyo, kamishna huyo alisema kuwa maafisa wa usalama watalazimika kutumia sheria na mbinu nyinginezo kuyakabili magenge hayo ambayo yamekuwa yakiwahangaisha wakaazi.

Achoki amewashauri vijana hao kujisalimisha kwa hiari kabla ya maafisa wa usalama kutumia nguvu.