Polisi wilayani Likoni wanasema wamekamata genge la washukiwa wa uhalifu wanalosema ni la “Kapenguria six” linalohusishwa na kuhangaisha watu na pia uporaji wa mali eneo hilo.
Kulingana na polisi, washukiwa hao wamekamatwa katika ufuo wa bahari wa Shelly beach baada ya kushambulia watalii, kuwapora mali na pia kuwajeruhi kutumia visu.
Mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa siku ya Alhamisi alitoa majina ya washukiwa hao kama Steve Owiti, David Murage, Mwalimu Suleiman na Brian Murage.
Marwa amesema wamewanasa na mikufu ya dhahabu, kadi ya atm, na simu ya mkono na vitu vingine kadhaa amayo wana amini ni za wizi.
Washukiwa hao ambao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Likoni huku uchunguzi dhidi yao ukiendelea, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili mashtaka dhidi yao yafunguliwe.