Baadhi ya wahanga wa ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-08 wameelekeza kidole cha lawama kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya jinai, Luis Moreno Ocampo, kwa kufanya uchunguzi hafifu.
Walisema uchunguzi hafigu alioufnya Ocamp umepelekea kesi dhidi wa viongozi wa Kenya kukosa uzito wa kisheria huku washukiwa wakiachiliwa huru mmoja baada ya mwingine.
Waathiriwa hao wamesema hawana matumaini kwamba mahakama hiyo itawapa haki licha ya kupoteza mali ya thamana isiyojulikana katika machafuko hayohuku zaidi ya watu 1,500 wakipoteza maisha yao.
Mnamo Ijumaa, kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya ICC ilitupilia mbali mashataka dhidi ya rais Uhuru Kenyatta, hatua ambayo imeibua hisia tofauti miongoni mwa Wakenya.
Mbunge wa Molo Jacob Macharia amesema mahakama hiyo imethibitisha kwamba haina ushahidi wa kuonyesha kuwa Rais Kenyatta alipanga na kufadhili ghasia zilizochipuka katika maeneo mbali mbali nchini.
Aliongeza kuwa Rais Kenyatta ameonyesha dunia nzima kwamba yeye anaheshimu utawala wa kisheria baada ya kuhudhuria vikao vya mahakama ya ICC bila kujali wadhifa wake.
Hata hivyo, wakimbizi hao wamedai Ocampo alivuruga taratibu za uchuguzi wa kesi wakisema ni heri kesi dhidi ya naibu rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang nayo isitishwe.
Aidha, wahanga hao wamesema mahakama za humu nchini pamoja na idara ya upelelezi hazijaonyesha nia ya kuwachukulia hatua washukiwa waliokamatwa wakati wa machafuko hayo pamoja na viongozi waliojumuishwa na tume ya jaji mstaafu Philip Waki kwa madai ya kuhusika katika uhalifu wa kivita.