Mwanzilishi wa kituo cha watoto mayatima na wajane cha 'Good Samaritan Widows Organisation' mchungaji Elias Karisa, amesema kuwa elimu ndio hazina kuu katika maisha ya mwanadamu.
Akizungumza katika kituo hicho, kilichoko eneo la Jomvu Mikanjuni, Kaunti ya Mombasa, Karisa aliwataka washikadau na wahisani mbali mbali kujitokeza na kuwasaidia watoto na wajane hao ambao wanaishi bila matumaini.
Aidha, mchungaji huyo alisema kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho kumesaidi pakubwa kwa kuwanusuru watoto wanao randaranda mitaani.
Vile vile, Karisa amewataka mbunge wa Jomvu pamoja na gavana wa Mombasa kuingilia kati kuona kwamba watoto hao wapatao 150 na wajane 100 wanasaidika sawa na Wakenya wengine.
Wanafunzi wa kituo hicho walisema kuwa wana matumaini kuwa wataweza kuorodheshwa katika awamu ya pili ya shule za umma katika kaunti zote 47 zitakazopokea vipakatalishi ili kuendeleza masomo ya teknolojia.